Watu kadhaa mbaroni kuhusiana na mashambulizi ya kutumia tindikali -Zanzibar
Jumatatu Polisi kisiwani Zanzibar , ilithibitisha watu 15 kutiwa mbaroni , kwa tuhuma
za kumshambulia kwa tindikali Padre Josseph Anselm Mwanagamba , Ijumaa iliyopita na
shambulio jingine la mwezi uliopita kwa walimu wawili wa kujitolea kutoka Uingereza.
Kamisheni wa Polisi Zanzibar , Mussa Ali Mussa, ameeleza kuwa, baadhi ya watuhumiwa
nii vijana waliokuwa wakitafuta mbinu za kuondoka kwa nia ya kwenda kujiunga na kikundi
cha uhalifu cha Somalia cha al Shabab. Na wamekiri kuwa walikuwa wanakwenda kujindaa
kwa jihad. Mussa amesema, Polisi bado inaendelea kuwachunguza watuhumiwa hao, na
mara kesi yao itatajwa mahakamani. Na kwamba bado ni mapema mno kujua lengo la mashambulio
hayo.
Jumapili , Rais wa Zanzibar , Dr Mohammed Shein, aliiagiza Idara ya
polisi visiwani Zanzibar, kwa haraka, kufanya upelelezi wa kina juu ya mashambulio
haya ya kutumia tindikali na wahalifu wakamatwe na kufikisha mbeleya sheria mara moja.
Dr Shein alitoa agizo hilo, wakati akimtembelea Padre Anselmo Mwangamba aliyemwangiwa
tindikali na mwili wake kudhurika na kulazwa katika hospitali ya hospitali ya mnazi
mmoja mjni Zanzibar.
Dr Shein alisema , shambulio kama hili ni unyama wa hali
ya juu kufanyika katika jamii iliyostaraabika , na hivyo serikali yake haiwezi kuwavumilia
wahalifu kama hao. Na aliwataka Wakatoliki na wakristu kwa ujumla na watu waliostraabika,
kuwa na uvumilivu , wakati serikali inalishughulikia suala hili.
Padre Mwanagamba
kwa wakati huu amelazwa katika wodi ya Kibasiri ya Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya
Muhimbili, iliyoko jijini Dar es Salaam.
Na Kesi ya Ponda yaahirishwa
hadi Oktoba Na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro imemnyima dhamana
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, anayekabiliwa
na mashtaka ya kukaidi amri halali, kuharibu imani za dini, kushawishi na kuchochea
vitendo viovu katika jamii.
Ombi la kumnyima dhamana lilitolewa na Wakili
wa Serikali, Bernad Kongola, akidai kuwa DDP kwa sababu ya maslahi ya nchi na usalama
wake mwenyewe.
Ombi hilo lilisababisha mvutano wa kisheria kati ya upande
wa mashitaka na upande wa utetezi hali iliyomfanya Hakimu Kabate kuahirisha kesi hiyo
hadi Oktoba mosi, ili kupitia vifungu vya sheria kuona uwezo wa kusikiliza shitaka
hilo ama shitaka hilo lifunguliwe katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbali
ya kuimarishwa ulinzi katika eneo la Mahakama, pia barabara zinazokatisha mahakamani
hapo zilifungwa hali iliyosababisha kusimama kwa muda kwa shughuli katika ofisi za
serikali zilizopo mahakamani hapo ikiwemo ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ofisi ya Hazima
Ndogo na Madini.
Wafuasi wa Ponda, kabla ,katika msikiti wa Mungu Mmoja
Dini Moja uliopo katika eneo la Kiwanja cha Ndege, walifanya mkesha wa itikafu iliyosomwa
kwa ajili ya kuomba kiongozi huyo ashinde kesi inayomkabili.