Mapadre wa Roma wanampenda Mungu, wanaupenda utume wao na ni waaminifu katika kazi
yao ya kichungaji huku wakipenda na kuwa karibu na wote wanao hitaji huduma zao. Haya
yamesemwa na Cardinali Agostino Vallini, Vika wa Roma alipokuwa akimkaribisha Baba
Mtakatifu Francisco kwenye jumuiya ya mapadre wa Roma wakati wa Mkutano na Papa siku
ya Jumatatu kwenye kanisa Kuu la Mtakatifu Yohanne Laterano lililoko mjini Roma.
Alisema
Mons. Valinni kwamba Mapadre wanatajirika na kupata nguvu mpya kwa maneno na matendo
ya Khalifa wa Mtakatifu Petro, Papa Francisko tangu kuchaguliwa kushika wadhifa huo
Mwezi Machi mwaka 2013.
Mons. Vallini ameutaja ukakamavu na unyenyekevu wa
Baba Mtakatifu Franscisko pamoja na jitihada zake za kuwa karibu zaidi na maskini
na wale wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii kama mambo ya kutia moyo na ambayo yamegusa
mioyo ya watu wengi. Mons. Vallini amesema kwamba Papa amekuwa ni alama ya nyakati
ambayo Mungu ameupatia ulimwengu na ambayo Mapadre wanapaswa kuiona kama mwaliko wa
kujirudi na kuyahuisha upya maisha yao na mwaliko wao wa kumfuasa kristo kwa karibu
zaidi.
Naye baba Mtakatifu ameendelea kuwaasa wanae wapendwa mapadre akisema
kwamba kanisa linao watakatifu wengi mbali na changamoto za hapa na pale, na kwamba
utakatifu huo ndio wa kupewa kipaumbele cha kwanza, utakatifu wa kuish maisha ya kawaida
kiaminifu kama wafanyavyo wamama na wanawake na wanaume watakatifu wengi sana duniani
wanaoendeleza familia zao bila ya kujishaua. Ni utakatifu huo unaoliimarisha kanisa,
anasema Papa, na kwamba sio kutenda mambo yasiyo ya kawaida au kuonyesha ujasiri
mkuu kunakomfanya mtu kuwa mtakatifu, bali kuyaishi kiaminifu na kikamilifu maisha
ya kila siku na changamoto zake zote.