2013-09-17 09:45:11

Masista waliotolea mhanga maisha yao Algeria- wakumbukwa ..


Masisita wawili wamissionari wa Shirika la Mtakatifu Augustine , waliouawa mwaka 1994 wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe Algeria , wamekumbukwa kwa sala na maombi na jumuiya yao, kwa uaminifu wa majitoleo katika huduma Injili na imani hadi hatua ya kuuawa.

Shirika la Habari Katoliki kwa Afrika (CISA) , hivi karibuni lilitaaarifu kwamba, Sister Caridad Alvarez na Sista Esther Paniagua , waliuawa wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya Algeria na vikundi vya Maasi vya Kiislamu wasiovumilia wengine , ambao walikuwa wakilenga vikundi vingine vidogovidogo kama chambo katika machafuko hayo na hasa wageni .

Vita hivyo vya karibia miaka kumi vilianzishwa mwaka 1991 , kwa makali zaidi mwaka 1994 ambamo balozi zilishauri wageni walioingia Algeria kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo. Masista wa Shirika la Mtakatifu Augustine wakiwa wamekabiliwa na changamoto hiyo, Mkuu wa Shirika Kijimbo , Sista Maria Jesus Rodriquez, alitembelea jumuiya tatu za shirika zilizokuwa Algeria licha ya hali ya ghasia za mapigano kuwa mbaya, ambako alikwenda kwa nia ya kuwashauri Masista waondoke.

Aidha Askofu Mkuu wa Algiers, aliungana na ombi la Sista Maria Jesus, kuwataka watawa, waone hatari zinazo wakabili, na waaamue kwa hiari kamili, kutenda kama dhamiri yao inavyowatuma au wabaki au waondoke na kurejea makwao.

Masista wengi , walitoa maamuzi ya kubaki katika uaminifu wa majitolea ya kuhudumia Injili , na kwa ajili ya upendo waliokuwa nao kwa watu wa Algeria kwamba walipenda kuendelea kushirikishana nao imani kupitia shuhuda za maisha na hivyo hawakupenda kuondoka badala yake wateseka na watu hao.

Jibu la wengi likiwa, maisha yao yako mikononi mwa Mungu, na anajua hitima ya maisha yao. Si kwamba walipenda kufa lakini walipenda kuendelea na kuihudumia Injili ya upendo kwa watu wote. Kwa kishawishi hicho Masista Caridad Alvarez na Sista Esther Paniagua ,ni kati ya Masista 19 waliouawa kati ya mwaka 1994-1996, akiwemo Askofu Pierre Claverie wa Jimbo la Oran aliyeuwa pamojana dreva wake kwa kulipukiwa na bomu akiwa nyumbani kwake.








All the contents on this site are copyrighted ©.