2013-09-16 15:11:22

Shirika la Don Orion lakamilisha sinodi yake


Shirika la Don Orion limefanya mkutano wake wa Sinodi kwa wanachama wake wa Afrika. Sinodi hiyo imefanyika mjini Bonoua, nchini Ivory Coast kuanzia tarehe 8 hadi 10 mwezi Septemba 2013. Mkutano huo wa siku tatu umejumuisha wawakilishi wa wanachama wa shirika hilo kutoka nchi za Togo, Burkina Faso, Kenya, Msumbiji, Madagascar na Ivory Coast yenyewe.

Mkutano huo uliohudhuriwa na wanachama wapya 18 waafrika, na wanovisi 19, umeangazia maswala mbalimbali ya maisha ya jumuiya hiyo, yakiwemo maswala juu ya tamaduni na roho ya shirika la Don Orion barani Afrika. Pia mkutano huo uliangazia malezi na uhalisi wa maisha ya jumuiya, maana hasa ya umaskini na huduma za huruma, kwenye mazingira ya bara Afrika na maisha ya kitawa katika nyanja za mtu binafsi, jumuiya ya kitawa na jamii kwa ujumla.

Waliohudhuria mkutano huo wameweka malengo ya kutafuta mbinu muafaka za kuendeleza sura ya shirika la Don Orion kwenye mataifa yanayoonyesha hamu ya kushirikiana na shirika hilo na hasa zaidi kwenye nchi za bara Afrika. Mambo yatakayotiliwa mkazo kwenye mahusiano hayo ni pamoja na malezi ya awali, na uhusiano na shirika hilo kwa ujumla.

Shirika la Don Orion limekuwa na ongezeko ya idadi sio tu ya wanachama, bali pia nyanja mpya za huduma za huruma na kichungaji zenye kutolewa na shirika hilo. Hivi karibuni shirika hilo limeanzisha jumuiya mpya 5 na vituo vya huduma za kijamii na kiroho kwenye mataifa ya Burkina Faso, Togo, Kenya na Madagascar, pamoja na kituo cha walemavu mjini Maputo, Msumbiji. Pia sasa kuna watawa wa kike wa shirika hilo wanaondesha zahanati na kutoa huduma za afya kwa jamiina hasa akina mama wajawazito nchini Madagascar.

Proggetti zingine zinazoendelea kushughulikiwa na shirika hilo ni pamoja na Senta ya kuwapokea wageni mahujaji wa madhabahu ya “Bibi Yetu wa Garde" , mjini Bonoua, Ivory Coast, na seminari mjini Maputo, Msumbiji.

Mkuu wa shirika hilo, Padre Flavio Peloso abasema kwamba mkutano huo ulipewa jina la Sinodi ili kuonyesha ukuu wa mkutano huo, ambao unamaanisha wakuu na wanachama wa shirika kutafakari kwa pamoja umahiri na mwelekeo wa shirika kwa mtazamo wa tamaduni na maisha ya kitawa barani Afrika.








All the contents on this site are copyrighted ©.