2013-09-13 15:53:29

Familia ni zaidi ya nadharia za maisha bali ni...


Mustakabali wa jamii, umesimikwa katika utendaji wa sasa wa wazee na Vijana. Ni ujumbe wa Papa kwa washiriki wa adhimisho la 47 la Wiki la Jamii Katoliki nchini Italy. Papa amewakumbusha kwamba, kwa jamii ya Wakristu, familia ni zaidi ya nadharia nyepesi ya kujadiliwa , ila ni mfumo thabiti wa maisha, kwenye utendaji wa kila siku, ni njia na mapito ya kizazi hadi kizazi , ambamo imani huenezwa na kudumishwa kwa upendo na tunu msingi za maadili.

Familia ni mshikamano thabiti ni mahali pa kazi , uvumilivu na pia mahali pa kujenga matumiani na upendo . Yote haya, jumuiya ya Kikristu, inapaswa kuyaishi katika mwanga wa imani, matumiani na upendo , na kamwe jumuiya ya Kikristu haipaswi kujitenga au kujifungia yenyewe, lakini daima ni kujichanganya na wengine na hivyo kuwa chachu ya matendo mema katika jamii na kwa ajili ya ukuzaji wa mazuri kwa watu wote.

Wiki la Wakatoliki Italiy lilianza Alhamisi 12 hadi 15 Septemba 2013. Kitaifa sherehe zinafanyika Turin Kaskazini mwa Italy, chini ya Mada : Familia: Matumaini na mustakabali wa Jamii ya Italy.

Papa amewataja vijana katika umri wao, wanao uwezo na nguvu za kuendeleza majiundo bora kwa watoto wao . Nao wazee wakiwa wanaishi kwa kumbukumbu za maisha yao, hufundisha uzoefu wao kwa vijana yapi yanafaa na yapi yanaweza kumtumbukiza mtu katika dimbwi la matatizo.

Papa ameonya jamii isiyowafikiria wazee , watoto na vijana, ni jamii iliyo katika hali ya kutoweka, na wala haina mustakabali, kwa kuwa hutumia vibaya yote mawili, kumbukumbu za wazee na matazamio ya vijana kwa siku za baadaye. Papa alieleza kwa kuangalisha katika dhana za familia, kama ilivyotajwa katika Kitabu cha Mwanzo, iliyosimikwa katika misingi ya Mke na mme wataungana na kuwa kitu kimoja na kuzaa watoto.
Na hivyo ni lazima kusisitiza hili kwamba , familia hii ya mke na mme ndiyo msingi wa jamii na utendaji wake wote katika hatua zote za kiuchumi kwenye kipimo cha binadamu , na hivyo inahitaji kuungwa mkono na kusaidiwa katika kila hali. Papa alieleza na kuonyesha kujali matatizo ya watu yanayolikabili bara la Ulaya.

Amesema si rahisi kupuuza mateso yanayokumbana na familia nyingi leo hii kutokana na ukosefu wa ajira, ukosefu wa makazi na changamoto nyingine nyingi , zinazopambanisha uhuru kamili wa mtu kuchagua kile anachopenda kufanya. Pia familia zinateswa na marubano ya ndani kati ya wanandoa, na hivyo huvunja mnyonyoro wa malezi bora kwa watoto na badala yake watoto huishia kuona migawanyiko na utengano , ghasia na vurugu ambazo huharibu mshikamano unaopaswa kuwemo ndani ya familia. Katika yote haya, kuna haja ya kutafuta kila linalowezekana kwa heshima na maana kamili ya mshikamno na udugu, kama msaada kuisaidia kila familia, inayoanzishwa ya mke na mme inapata mahitaji yake na hivyo kusimama imara kimaisha.

Papa alikamilisha ujumbe wake akisema, pamoja na hayo si rahisi kuacha kuwataja wale ambao kupitia maisha ya kawaida lakini mazuri yenye furaha na imara ambayo hushuhudia uzoefu wao katika ndoa na uzazi kwa furaha zote , wakiangaziwa na kudumishwa na neema za Bwana bila woga katika kupambana na misalaba na majaribu mengi katika muungano wao, wale ambao kamwe hawaachi kutembea katika njia ya upendo , wakiimarishana kwa nguvu zaidi na kwa ukamilifu zaidi.








All the contents on this site are copyrighted ©.