2013-09-12 15:16:07

Papa ajibu maswali ya mtu asiye amini kwa Mungu


Papa ajibu barua ya mtu asiye amini kwa Mungu, akisema , leo hii , majadiliano na wasio amini kanisa, ni nafasi nzuri na chanya , tena muhimu na ni tunu ya thamani sana, kwa ajili ya Kanisa. Asiyeamini anapouliza maswali, ni jambo jema kwake kwa kuwa anautafuta ukweli . Na hiyo huu unakuwa ni wakati muafaka kwa kanisa kufungua milango katika mfululizo wa mijadala na midahalo, kwa ajili ya kuuzamisha mwanga wa ukweli wa imani ya Mkristu kwa wengine wasioamani . Yanakuwa ni majadiliano msingi, hakika na ya kweli yailyo simikwa katika ukweli wote.

Ni majibu ya Papa Francisko, akijibu maswali yaliyotumwa kwake kupitia barua ya wazi na aliyewahi kuwa mhariri wa Gazeti la "La Republica" la Italy, Eugenio Scalfari ,mwenye umri wa iaka 89 , kati ya maswali yake, alitaka kujua iwemo mtu asiyekuwa na imani kama yeye akitenda dhambi husamehewa na imani ya Kristu. Na je , Ukweli halisi upo? Na fikra juu ya uwepo wa Mungu si tu kwamba ni mawazo ya akili ya binadamu?

Papa Francisko, katika majibu yake yalichapishwa katika gazeti la Republica Jumatano(11.09.2013),na pia gazeti la Vatican la L'Osservatore Romano, amehimiza wasio amini, kutafuta muda na kuwa na midahalo na majadiliano ya kirafiki yaliyo wazi katika kuupata ukweli . Papa amesema kwa kadri karne zinavyopita, tangu Ukristu kuanza, wengi wanamezwa na mawazo kwamba , imani na ukristu ni mambo ya kufikirikafikirika tu katika akii ya binadamu kitu kisichoeleweka , ni giza na ushirikina. Lakini kumbe ni kinyume chake, Ukristu ni nuru inayomulikia katiak kuuona ukweli halisi wenye kuwaokoa watu kutoka giza nene la kutojua hatima yao . .Papa ameeleza kwa kunukuu baaadhi ya maandishi vilivyomo katika waraka wake wa kichungaji wa hivi karibuni, “ Mwanga wa Waamini, Lumen Fidei”, ambamo mna msisitizo kwamba, imani kamwe si uzushi au majigambo, lakini ni unyenyekevu unaoruhusu muumini kujenga mahusiano ya k aribu zaidi na wengine. Imani kwa Mungu ni upendo kwa watu wengine.

Scalfari katika tahariri zake mbili za Julai 7 na Agosti 7, alitoa maoni yake akionyesha kusadiki kwamba, imani ni utamaduni na hisi tu za kufikirika za maadili ya dini ya Kikristo, hivyo msamaha wa Mungu hauwahusu wasioamini Mungu.
Papa amejibu akisema, huruma ya Mungu haina mipaka , na huwafikia wote wanaoitafuta kwa moyo mkujufu, hata kwa wale wasiomini Mungu, ndani mwao mna dhamiri inayodai utii, Papa anaandika.
Na kwamba dhambi ipo hata kwa wasio na imani, alionya, mtu yoyote hutenda dhambi pale, pale anapokataa kutii dhamiri. Dhambi zote ni kutenda kwenda kinyume na dhamiri. Daima kuna sauti katika moyo wa mtu inayodai kuutiii wema na kuukataa mabaya. Haya ni kweli ni mahojiano ya ndani ya moyo, yanayotakiwa kutolewa maamuzi , kabla ya kutenda. Baahati mbaya Uamuzi huu huchezwa au kupuuzwa katika kuchagua kati ya wema au ubaya katika utendaji wetu wa kila siku. .
Pia Papa akijibu swali la Scalfari iwapo binadamu anapofariki basi pia mahusiano yake na Mungu hutoweka, , amesema , Mkristu anasadiki roho ya mtu haipotelei , anapokamilisha maisha ya hapa duniani, bali huingia katika dunia ingine tusiyoweza kuiona kwa macho na akili yetu ya kibinadamu, Hili ni fumbo ambalo binadamu haweza kulitangua kwa akili yake , isipokuwa kwa Yeye yule aliyeumba ulimwengu. Maandiko Matakatifu yanasema, Mungu aliiumba mbingu mpya na nchi mpya , wakati wa kuhitimisha kazi yake , kwa wale wenye imani, husubiri kwa hamu kurejea kwa Bwana mara ya pili, kwa ajili yetu sote.

Papa aliendelea kutafakari juu ya asili ya Imani ya kikristu katika mahusiano na dini zingine na hata wasioamini , akisisitiza kwamba, utendaji wa Yesu uliotuwezesha sisi wote kuwa wana wa Mungu , wake kwa waume, pia humwezesha Mkristu kuwa na uhusiano wa karibu na watu wote, kwa kuwa watu wote wameumbwa na Mungu mmoja kwa sura na mfano wake, Mungu aliye upendo. . Na hivyo inakuwa wajibu muhimu kwa kila binadamu kuufahamisha upendo wa Mungu kwa watu wote, si katika njia za majigambo na kifahali , lakini kupitia unyenyekevu wa moyo na huduma kwa watu wote na hasa wale waliowekwa pembezoni na jamii.

Papa ameandika katika barua yake kwa Scalfari kwamba, kwake imekuwa ni heshima na amefurahia kuulizwa maswali hayo , na kwa furaha hiyo hiyo yuko tayari kuulizwa tena na kutoa majibu yake kwa uaminifu wa ukweli wote anaoufahamu yeye. Na kwamba ameichukulia barua ya Scalfari, kuwa mwaliko wa waaamini wake wanaendelea kutembea pamoja katika kumtafuta Mungu na kuishi nae. Anaamni Kanisa , licha ya madhaifu yake , makosa na dhambi zinazoweza kutendeka ndani yake, bado nia na azima na kusudi lake kuishi na kumshuhudia Yesu Kristu , kuwa ndiye Yeye, aliyetumwa na Baba , kuleta habari njema kwa maskini, kuwatangazia mateka na vipofu , kuwaweka uhuru wale wanaoonewa, na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana" (Lc4, 18-19) ".


Mwisho Papa kwa heshima kuu alionyesha heshima zake kwa dini zingine na urafiki uliopo na Wayahudi na wale wote aliofanya kazi nao kwa ukaribu akiwa katika nchi yake ya Argentina . Alitafakari juu ya matendo maovu kama yaliyo tokea katika kambi za kiyahudi wakati wa vita vya dunia, akisema , hakuna maneno yanayoweza kutosha kuwashukuru Wayahudi kwa kuidumisha imani yao kwa Mungu , ambayo hutufundisha sisi daima kubaki katika umoja na mshikamano wazi na upendo usiokuwa na miisho na wengine wote.

Carlo Di Cicco Naibu Mkurugenzi wa Gazeti la L’Osservatore Romano , akitoa maoni yake juu ya majibu ya Papa Frfancisko , ameonyesha kuyafurahia majibu kwamba, yanaonyesha vyema maana ya mshikamano wa Kanisa. Hivyo , majibu ya Papa Francisko ni mwaliko ka wote wanaotafuta kuujua ukweli wa kanisa , kwamba ni mkusanyiko wazi wa watu wote , pia kama njia ya majadiliano kwa manufaa ya wote.










All the contents on this site are copyrighted ©.