2013-09-12 15:37:22

Kampeini ya UNICEF kuwezesha watoto kupata elimu shuleni


Serikali ya Somalia imeanzisha mchakato wa kampeni ya kuwawezesha watoto millioni moja kupata mafunzo ya awali shuleni. Mchakata huo ulizinduliwa kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Masomo ya awali zilizofanyika hivi majuzi nchini humo kwenye miji ya Mogadisho, Garowe na Hargeisa.
Kampeni hiyo inaendelezwa na idara ya elimu ya Somalia ikishirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watoto, UNICEF, na mashirika mengine ya kimataifa, itakayoendeshwa ndani ya miaka mitatu inalenga kuwapa fursa robo ya watoto wenye umri wa kwenda shuleni lakini ambayo hawajapata fursa ya kujiandikisha kwenye mfumo wa elimu nchini humo.
Ada ya kujiunga na shule ya msingi nchini Somalia ni moja ya ada zilizo chini zaidi ulimwenguni. Hata hivyo, kati ya kila watoto kumiwenye umri wa kuwa shuleni, ni watoto wanne tu walio shuleni. Watoto wengi sana pia hujiunga na shule ya asili wakiwa wamepitisha umri halali wa miaka sita, ilhali wengine wengi hulazimika kuachia masomo njiani, kabla ya kumaliza shule.
Hali hii inaathiri hata masomo ya sekondari kwani watoto wanaohitimu kujiunga na shule za sekondari ni wachache sana. Nayo idadi ya wasichana huwa ni ndogo zaidi kwani wengi wao huachia masomo katikati.

Kutokana na changamoto hizi, Kampeni hiyo inalenga kuwafaidi watot millioni moja wenye umri wa kati ya miaka 6 na 13. Wakati huohuo kampeni hiyo pia itatoa mafunzo kwa ajili ya kuwapa ujuzi watoto walio na umri wa juu kuliko walengwa wa masomo ya awali yaani miaka 14 hadi 18 ili kuwaepusha na uwezekano wa kujiunga na vikundi vya kihalifu.

Msemaji wa UNICEF nchini Somalia Bw. Sikander Khan anasema kwamba kampeni hiyo inayojulikana kama Nenda Shuleni, ni ya msingi na ni kama ufunguo kwa Somalia ya siku za usoni, kwani vijana waliosoma ni mtaji mkubwa kwa uendelezaji wa amani na usalama nchini humo.
Kampeni hiyo itagharimu zaidi ya laki moja na kumi na saba ya dola za kiamrekani. Siku ya kimataifa ya elimu ya awali ilianzishwa mnamo 1965 na huadhishwa kila mwaka ifikapo tarehe 8 Septemba.










All the contents on this site are copyrighted ©.