2013-09-12 15:30:21

Jamhuri ya Afrika Kati yatuma ujumbe wake Roma kwa ajili ya kutafuta amani.


Jamhuri ya Afrika ya Kati sasa imetuma wajumbe wawakilishi kwenye mkutano wa kutafuta suluhisho la amani kufuatia migogoro na kinzani za kivita vinavyoendelea nchini humo. Ujumbe huo wa wawakilishi kutoka serikali, na uwakilishi kutoka kamati ya kitaifa kwa ajili madaraka, na wawakilishi kutoka jumuiya za kidini na vyama vya kijamii.
Habari zilizochapishwa kwenye Shirika la Habari la ANSA linasema kwamba kundi hilo la wawakilishi kutoka Jamhuri Ya Afrika ya Kati, liko nchini Italia na siku ya Jumatano wamekutana na Katibu msaidizi wa mambo ya nje wa Italia, Mario Giro.
Ujumbe unalenga kuzungumzia mikakati muafaka kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Jamhuri ya Afrika ya Kati inapata amani na uongozi unaojali haki za kibinadamu na maendeleo ya watu wake. Mwenyejiwa mkutano huo ni jumuiya ya Mtakatifu Egidio iliyochaguliwa na rasi wa mpito wa Afrika ya Kati, Bw. Michael Djotodia.
Jumatano ujumbe huo, ulitialiana sahihi na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na kundi hilo kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, mkataba wa kushirikiana ili kuweza kupata suluhisho la amani na usalama, kufuta migogoro iliyoikumba nchi hiyo.











All the contents on this site are copyrighted ©.