2013-09-11 15:53:51

Tweet, Papa ashukuru wote walio shiriki mkesha wa sala ya kuombea amani.


Ujumbe wa Papa kwa siku ya Jumanne , kupitia ukurasa wa tweet @ pontifex, umetoa shukurani za dhati kwa wote walio shiriki mkesha wa sala ana mafungo kwa ajili ya kuombea amani Syria na duniani kote.
Kama ilivyokuwa Jumapili, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Papa ameendelea kutoa ombi lenye kuwataka watu wote wakazane kuombea amani Syria , Mashariki na kati na duniani kote. Amesema vita pekee tunayopaswa kupigana nayo kwa wakati huu , ni mapambano dhidi ya dhambi na maovu.








All the contents on this site are copyrighted ©.