Papa ahimiza wenyeji kuwa na ukarimu wa ziada kwa wageni wahamiaji na wakimbizi
Papa Francisko Jumanne jioni,(10.9.2013) alikitembea kituo cha wakimbizi cha Astalli
hapa Roma kinachosimamiwa na shirika la Wajesuit kwa ajili ya wakimbizi (JRS). Akiwa
mahali hapo aliuita wingi wa mchanganyiko watu wenye asili mbalimbali na dini mbalimbali
kuwa ni utajiri unaopaswa kupokelea kwa mikono miwili, bila woga wala mashakamashaka.
Papa alisema kuna haja gani ya kuogopaogopa, iwapo imani ya kila mmoja ni
thabiti? Ni nini hasa cha kuogopa? alihoji Papa. Papa aliutumia pia muda huo, kutoa
shukurani zake za dhati kwa wafanyakazi na watu wa kujitolea kwa wema na ukarimu wao,
katika majitoleo hay ya bila kujibakiza katika kuutumia pia muda mwingi kusaidia maelfu
ya wakimbizi wanaopita katika milango ya kituo hicho kila mwaka , na kwa utambuzi
wao kuwa hawa ni watu , na kufanyakazi kwa bidii kwa ajili ya kupata majawabu katika
mahitaji yao.
Papa amelitaja jiji la Roma kuwa ni kituo cha pili kwa wakimbizi
wengi wanaoingia Italy, kupitia mlango wa Lampedusa, wa Kusini mwa Italy. Na aiielezea
safari yao watu hao tokea Afrika Kaskazini, kuwa ni ya kuchosha, zaidi ya yote ni
watu wanao tafuta kuboresha hali yao ya maisha kwa ajili yao na watoto wao . Papa
aliwaonea huruma zaidi wanawake na mama wengi wanaoanza safari hizi za kutafuta
ahueni za maisha, kwa ajili yao na familia zao, bila ya kujali changamoto ngumu mbele
yao.
Papa aliendelea kuonyesha kujali hali za wakimbizi na wahamiaji akihoji
ni mara ngapi habari za madhulumu na kukosa msaada kwa watu hawa zimesikika , licha
ya wengine kuwa hata hati halali ya ulinzi wa kimataifa au kuwa hati zinazo waruhusu
kuishi katika Jiji la Roma, lakini bado watu hao wanalazimika kuishi katika mazingira
mabovu na duni, ya kutisha , yenye kudharirisha utu wao na bila hata ya kupewa mwanya
wa kufikiria juu ya hali yao ya baadaye!
Kwa hali hizo, Papa alipeleka mawazo
yake kwa utume wa Wajesuit katika kituo cha Astalli, na kutoa pongeza kwamba, huduma
yao ya kuwapokea na kuwakaribu wahitaji, wakiwa wamemezwa na roho ya msamaria Mwema
na uelewa mpana , wanawainamia wenye shida na dhiki na kuwapa mkono wa karibu bila
kuhesabu faida au kuwa na woga . Hii ni sehemu ya mshikamano, akilitaja neno mshikamano
kwamba kwa wengine linaleta hofu hasa katika dunia iliyoendelea, uwepo wa woga, hata
kulitamka, kama vile ni neno baya. Lakani kumbe ni neno linalopaswa kuwa kinywani
mwa wote, Papa alisisitiza. Kisha Papa alionyesha hamu yake kwamba, ziara yake
hii katika kituo cha wakimbizi cha Astalli, na iitawweza kugusa mioyo ya wakazi wote
wa Jimbo la Roma na kichocheo cha kutafakari jinsi wanavyoweza kutoa jibu kwa wito
wa YesU Kristu, kuhudumia wahitaji , na bila ya kuukimbia uso wa mtu anayetafuta haki
. Na hii haimanishi tu kuwa mwema katika kutoa misaada kama chakula kwa mtu mhitaji,
lakini pia ni kuwasaidia waweze kusimama tena, katika njia ya maisha ya kawaida yenye
hadhi na heshima kamili. Papa alisisitiza huruma ya kweli , hudai haki, na Kanisa
katika Jimbo la Roma na taasisi zake , linapaswa kuhakikisha hakuna yeyote katika
Jiji hili anayekosa mlo wake wake wa kila siku au makazi au msaada wa kisheria katika
kuzitambua haki zake za kuishi na kufanyakazi kama binadamu mwingine yoyote. Ni mshikamano
wa kijamii unaodai utendaji wa haki kwa kila mtu. Papa pia aligeukia nyumba
za watawa watawa wa kike ambazo hazina tena watu , kwa ukarimu, kufungua milango kwa
wakimbizi na kwamba Kanisa halihitaji nyumba hizo za watawa zisizokuwa na miito,
kugeuzwa mahotel kama kitega uchumi cha kujipatia fedha. Hilo si lengo la Kanisa.