Papa akutana na walei wawakilishi wa vyama na jumuiya za kikanisa Italy
Jumatatu, Papa alikutana na wawakishi kadhaa wa vyama na jumuiya za kikanisa akiwemo,
Rais wa jumuiya ya Uhuisho mpya wa Kiroho, Bwana Salvatore Martinez, Rais wa Chama
Katoliki cha Italia , Franco Miano , pia Rais wa jumuiya ya uhuisho wa kiroho katika
udugu na upendo, Mateo Caliisi na bibi Michelle Moran, Rais wa Kitaifa kwa jumuiya
ya uhuisho mpya wa Roho Mtakatifu. Wote wa Italy .
Papa katika mazungumzo
na Salvatore Martinez, Rais wa Jumuiya ya Uhuisho Mpya wa Roho Mtakatifu, aliikumbuka
ziara yake ya kichungaji ya kimataifa ya hivi karibuni, Rio de Janeiro, akisema
ulikuwa ni mkutano wa Kipentekoste, ambamo walipata nafasi ya kuzungumza, katika
muono wa neema mpya katika njia za wokovu. Mkutano ulioweza kuwakutanisha vijana
toka pande zote za Dunia , waliofika usikiliza Neno la Mungu na kuliishi katika umoja
na mshikamano wa kikanisa. Papa ameonyesha kufurahi kwamba, kuna juhudi nyingi nzuri
zinazo fanyika kwa ajili ya Mabadiliko chanya ndani ya Kanisa na dunia, Na hivyo Papa
alionyesha ukaribu wake na vikundi hivi vya uamusho katika Kanisa.
Rais Martinez,
mara baada ya kukutana na Papa, aliwasilisha zawadi zilizoandaliwa na vijana wafungwa
wa zamani , ambao kwa sasa hujishughulisha na vijana ambao bado kifungoni, katika
Kituo cha Malezi Bora cha Polo, Mario na Luigi Sturzo, na pia zawadi kutoka wa wahamiaji
wa Lampedusa ambao kwa sasa wamehamishiwa Sicily. Ni zawadi zilizotengenezwa kwa
udogo wa kauri zilizosindikwa katika kituo hicho cha Sturzo.
Na pia katika
mazungumzo yao, walifanya mapitio katika shughuli zinazo fanywa na jumuiya kwa manufaa
ya wahamiaji katika mji wa Lampedusa, wafungwa na kituo cha Malezi cha Sturzo, watoto
na familia katika Moldavia na kisha Kituo cha Kimataifa cha Familia ya Nazareti,
walicho kabidhiwa jumuiya ya Uhuisho Mpya wa Kiroho na ambacho Baba Mtakatifu tayari
anakifahamu. Papa alionyesha kuvutiwa na shughuli za Kiroho , majiundo mpya ya kiroho
na Uinjilishaji wa RNS , ambamo wanajumuiya wake wako tayari kupeleka Neno la Mungu
katika mataifa mengine.
Na pia walizungumzia Ukristu barani ulaya hasa haja
ya uinjilishaji mpya nchini Italia, na udumishaji wa juhudi za vijana na familia.
Na pia waliunga mkono juhudi za mradi , unaojulikana kama mraba 10 10 wa Amri za
Mungu , ambao utaanza rasmi Septemba 21, huko Palermo , ambamo Baba Mtakatifu, atatoa
ujumbe wake kupitia matangazo ya video, na utaweza kusikika katika miji kadhaa.
Baba
Mtakatifu ameomba kwa unyenyekevu mkubwa, daima kumkumbuka katika maombi yao , kama
hakikisho maalum na ukaribu wake wa kichungaji kwa jumuiya na pia kwa ajili ya utendaji
wa shughuli katika mipango ya baadaye na mipango yake mwenyewe binafsi.
Jumuiya
ya uhuisho mpya wa Roho Mtaktifu RnS, ina wanajumuia zaidi ya 200,0000, wanaounda
vikundi zaidi ya 1,900, hapa Italia.