Watawa 68 ni kati ya watu 522 watakaotangazwa kuwa wenye heri na Mama Kanisa hapo
tarehe 13 Oktoba 2013, mjini Tarragona Uhispania. Watu hao 522 ni wafia dini wa Hispania
wa karne ya XX. Haya yamebainika kutokana na ujumbe wake Askofu Mkuu wa jimbo la Burgos,
Mons. Francisco Gil Hellín utakaosomwa kwenye Maparokia yote jimboni humo hapo siku
ya Domenica, tarehe 8 Septemba, 2013.
Kwenye ujumbe huo, Mons. Gil Hellìn
amewaalika wakristo wote wa jimbo lake kuhudhuria sherehe hizo za kihistoria nchini
humo, akisema kwamba baadhi ya mashahidi hao wa imani walitoka kwenye majimbo ya Levante,
bastantes na Madrid; na Kataluña, Aragón.
Naye Baba Mtakatifu Francisko atawakilishwa
kwenye sherehe hizo na Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza
waamini kuwa wenyeheri na watakatifu ambazo.
Mons. Hellìi amesema kwamba Mama
Kanisa daima amesadiki kwamba wafia dini, ni watu waliomwaga damu yao kwa ajili ya
imani, ambayo ndio ushahidi wa juu zaidi wa mapendo, wanaunganisha kabisa Kristo na
watu wake. Kwa sababu hiyo wanaheshimika na kukumbukwa kwa namna ya kipekee sana (katiba
ya Sheria za Kanisa, na. 50).
Ni jambo la kutia moyo hasa kwenye mwaka huu
wa imani uliotangazwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI na ambaye anaandika
kwenye barua yake ya Kichungaji ya Mlango wa Imani (Porta fidei, n. 13) kwamba “mwaka
huu ni wakati muafaka wa kuirejea historia ya imani, ambayo imejaa mafumbo kwani ndaniyake
mmechanganyika utakatifu na dhambi”.
Kwa kuwakumbuka wafia dini hasa ndani
ya mwaka wa imani ni ishara kwamba Kanisa linatambua utakatifu wa wana wapenzi wa
Mungu waliojitoa kidete kwa mapendo na linawapa wote walio safarini moyo wa matumaini
wakitambua kwamba huruma ya Mungu imeishinda dhambi. Mwaka wa imani ni mwaka pia wa
neema na baraka kwa Kanisa na jamii nzima, na hivyo ni mwaliko kwa watu wote kuwatazama
wafia dini ambao ni mifano ya imani, ya mapendo na hata ya huruma ya Mungu kwa wanadamu.