Maaskofu Katoliki nchini Ghana wameitaka serikali na vyama vya upinzani , kufanyakazi
kwa ushirikiano na kutengeneza mazingira yanayofaa, vijana kupata ajira, kuepusha
matendo maovu, rushwa na ubadhilifu, ubabe wa kisiasa au kidini usiokuwa na kiasi
na kuenea kwa maradhi ya zinaa katika taifa pendwa la Ghana.
Tamko la Maaskofu
la Jumatatu, linahimiza wananchi wa Ghana , kujenga moyo wa mashauriano na maridhiano
kwa ajili ya uwepo wa mshikamano wa kitaifa kwenye uwajibikaji wa wote katika kutatua
kero na matatizo yanayo jirudia mara kwa mara, katika jamii.
Hati ya MAaskofu
imetiwa sahihi na Askofu Mkuu Joseph Osei Bonsu, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Ghana(CBCG). Ni tamko linalo onyesha uwajibikaji katika vipengere nyeti vinavyohitajika
kufanyiwa mapitio ya kina hasa katika taratibu za uchaguzi na marekebisho katika
Kaatiba na changamoto zingine ngumu zinazohusiana na taratibu za uchaguzi, nchini
humo.
Maaskofu wanatazamia Waghana wote wataweza kuitikia ombi la Maaskofu
kwa moyo wa hekima na busara , bila ya kujali hadhi yao kisiasa, kiitikadi, kidini
au asili za ukabila. Ni kufuta kutofautiana kwa nyuma na kusonga mbele na sura mpya
ya umoja na mshikamano wa kitaifa kwa ajili ya kudumisha amani Ghana.