Mipango ya ujenzi wa Kanisa la Kianglikan Gahini, yakamilka
Ujenzi wa Kanisa la Kianglikan la Gahini wilayani Kayonza Rwanda, utatumia kiasi
cha Fedha ya Rwanda billioni moja hadi kukamilika. Denisi Karera , Mkuu wa Kamati
kuu ya Kanisa , ambaye pia ni mkuu wa tume kwa ajili ya kazi ya ujenzi wa kanisa
hilo, ameleeza hivi karibuni kwamba , maandalizi ya ujenzi wa kanisa hilo karibu yamekamilika
na kazi zinatazamiwa kuanza tangu mapema Desemba mwaka huu. Ujenzi huo utachukua
takriban mwaka mmoja kukamilika.
Kwa wakati huu waamini katika eneo hilo wanatumia
kanisa dogo lililojengwa miaka 50 iliyopita na hivyo sasa halikidhi mahitaji ya Ibada
katika eneo hilo. Hata hivyo Kanisa hilo halitabomolewa lakini litatuzwa kama ssehemu
ya historia ya Ukristu katika eneo hilo.
Kiasi cha fedha kinachohitajika
kinapatikana kwa njia za michango na harambee ya waamini.
Akizungmza na gazeti
mahalian a New Times, Askofu Alexis Bilindabagabo wa Jimbo la Gahini , ambaye huwakilisha
viongozi wa kanisa katika Kamati kuu anasema Kanisa jipya, historia ya Kanisa itarithishwa
kizazi hadi kizazi. Na amewahiza waamini katika jimbo hilo kujitolea kwa moyo wa ukarimu
zaidi, kufanikisha miapngo ya ujenzi wa kanisa jipya kama inavyotarajiwa.