2013-09-02 14:45:25

Maombolezo :Askofu Moses Kulola wa EAG- Tanzania amefariki duniani .


Wakristu na watu wenye mapenzi mema nchini Tanzania wanaomboleza kifo cha Askofu Mashuhuri katika makanisa ya Assemblies of God Tanzania , Askofu Moses Kulola, aliyefariki dunia Alhamis Agosti 29 , 2013.

Hadi kifo chake , Askofu Moses Kulola, alikuwa ni Mhubiri maarufu, mwenye kuwa pia na karama ya uponyaji ,aliyeweza kuwa na mvuto katika mikutano yake ya hadhara, na hivyo aliongoa wengi kujiunga makanisa ya Assemblies of God, na ulokole wka ujumla, nchini Tanzania na nje ya Tanzania.

Askofu Moses Kulola ,alizaliwa Mwanza June 28 1928. Alibatizwa katika Kanisa la African Inland Church (AIC), Makongoro Mwanza mwaka 1950. Alipata masomo yake ya elimu ya msingi shuleni Ligisha. Baadaye alijiendeleza hadi kuwa Mhubiri maarufu Injili ndani ya Kanisa AIC, katika kanda ya Ziwa Victoria. Mwaka 1962, alijinasua kutoa AIC, na kuwa mhubiri wa kujitegemea , chini ya makanisa ya Assemblies of God. Hata hivyo baada ya kukosekana maelewano dani ya TAG, katikA miaka ya 1980 na mapema 1990, Kulola , alijinasua na kuwa mhubiri Injili wa kujitegemea, hadi alipofariki dunia katika Hospitali ya AMI jijini Dare salaam , Alhamis iliyopita.

Askofu Moses Kulola ameacha mke Elizabeth na watoto kumi, mmoja wao Daniel Kulola, amechukua kazi ya baba yake ya kuhubiri Injili.








All the contents on this site are copyrighted ©.