2013-08-31 17:29:42

Askofu Mkuu Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Jimbo la Papa


Baba Mtakatifu Francisko amekubali kwa mujibu wa sheria ya kanisa namba 354, ombi la kujiuzulu kuwa Katibu wa Jimbo la Papa , lililotolewa na Kardinali Tarcisio Bertone. Hata hivyo amemwomba aendelee kubaki na wadhifa huo hadi Oktoba 15, 2013.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko akamteua Askofu Mkuu Pietro Parolin, Mjumbe wa Kitume wa Papa nchini Venezuela, kuwa Katibu mpya wa Jimbo la Papa , na atachukua madaraka kamili ya ofisi hiyo hapo Oktoba 15, 2013.

Siku hiyo, Oktoba 15, 2013, Baba Mtakatifu, atakutana na Wakuu na maofisa wa ngazi za juu katika sekretariat ya nchi ya Vatican, na anatazamia kutoa shukurani zake za wazi, kwa Kardinali Tarcisio Bertone kwa ajili ya huduma yake, aliyoifanya kwa uaminifu na unyenyekevu mkubwa, kwa Kiti Kitakatifu . Pia Papa atatoa shukurani zake kwa yule anayeanza utume wake kama Katibu mpya wa Jimbo la Papa.

Askofu Mkuu Pietro Parolin mara baada ya uteuzi huo, kutangazwa rasmi katika vyombo vya habari, mara alitoa tamko lake, ambamo ameonyesha shukurani zake za dhati kwa Papa Francisko kwa imani aliyo ionyesha, kwamba ambayo anasema hastahili , na kwa mara nyingine, kwa kutambua nia , utendaji na uwepo wake kamili, katika utume wa Kanisa, chini ya maongozi yake kwa ajili ya utukufu Mkuu wa Mungu, fadhila na mema ya Kanisa Takatifu, maendeleo na amani ya binadamu, ili kwamba, ubinadamu uweze kuwa hoja msingi katika maana ya maisha na matumaini.

Na kwamba, anasikia nguvu mpya za neema ya wito huu , licha ya kuwa ni tukio jingine la kumshangaza katika maisha yake, na zaidi ya yote , uzito wa majukumu na wajibu unao wekwa mabegani mwake, kutokana na kazi hii mpya, zito na changamoto ngumu inayodhaminishwa kwake mbele ya mamlaka , yeye aliye dhaifu na maskini.
Kwa sababu hii, anajikabidhi mwenyewe katika upendo na huruma ya Bwana , ambaye hakuna jambo au mtu anaye weza kumteganisha nae, na katika maombezi ya wote. Pia ametoa shukurani zake kwa wale wote walio mwonyesha na wale wanaoanza kumwelewa na pia kwa wale wote watakaokuwa tayari kwa hali zote kumsaidia, ili kwamba kila mmoja aweze kuwa na moyo wa kutaka kumsaidia katika utume wake huu mpya.


Aidha amesema,” Mawazo yangu nayapeleka kwa familia yangu , na kwa watu wote ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu : katika parokia niliyozaliwa na nilizo hudumu na kwa jimbo langu pendwa Vicenza la Rome, na kwa nchi ambako nimefanya kazi , Nigeria, na Mexico , na hivi karibuni nchini Venezuela, ambako ninasikitika kuondoka. Na pia mawazo yangu nayapeleka kwa Papa Mstaafu Benedict XVI - ambaye aliniteua kuwa Askofu , na kwa Sekretarieti ya Jimbo Takatifu, , ambayo ilikuwa nyumbani kwangu, kwa miaka mingi, Na pia kwa kardinali Tarcisio Bertone , na wakuu wengine , wafanyakazi wenzangu, na wafanyakazi katika ofisi za Curia na kwa wale wote wanao mwakilisha Baba Mtakatifu na Jimbo la Papa kidiplomasia duniani kote. Kwao wote nina wiwa nao deni kubwa".

Askofu Mkuu Pietro Parolin anaendelea kutoa ahadi kwamba, atatumikia chini ya nguzo tatu , Injili , Kanisa na kwa Papa Francisko, kwa imani na utulivu, kama Papa alivyowataka tangu mwanzo wa utume wake, kutembea , kujenga na kuikiri imani katika umoja na mshikamano thabiti.

Askofu Mkuu Pietro Parolin, amemalizia wasaa wake kwa kuomba msaada wa Mama wa Yetu Mlima Berico , Guadalupe na Coromoto , awajalie wote , ujasiri wa kutembea katika uwepo wa Bwana na kwa Msalaba wa Bwana , wakilijenga kanisa la juu ya damu ya Bwana , iliyomwangika juu ya Msalaba , na katika kukiri utukufu moja wa Kristo aliyesulubiwa . Na kwa njia hii Kanisa litasonga mbele .

Maelezo binafsi ya Askofu Mkuu Parolin,
Alizaliwa Schiavon (Vicenza) 17 Januari 1955.
Alipadrishwa 27 aprile 1980 jimboni Vicenza. Ana shahada ya sheria za Kanisa, na aliingia katika utumishi wa kidimplomasia wa Jimbo la Takatifu , tarehe 1 luglio 1986, na kufanya kazi katika ofisi za Mjumbe wa Papa , nchini Nigeria, Mexico na katika kitengo cha Katibu wa nchi, kwa ajili ya mahusiano na nchi zingine na baadaye kuwa katibu Mwandamizi katika kitengo hicho cha Mahusiano na nchi zingine tangu 30 november 2002.
17 agosto 2009 aliteuliwa kuwa Nunzio wa Papa nchini Venezuela , na hivyo kupandishwa cheo na kuwa Askofu wa Mkuu wa jina wa Aquadipendente. Na alisimikwa katika cheo hicho na Papa Benedikto XVI , tarehe 12 settembre , 2009.

Pongezi
Mara baada ya uteuzi huu kutangazwa katika vyombo vya habari , Rais wa Italia, Giorgio Napolitano, alimtuma ujumbe wake wa pongezi kwa Askofu Mkuu Pietro Parolin, ambamo ameonyesha kupokea kwa furaha kubwa , habari ya uteuzi huu, unaohusu nafasi ya ngazi ya juu katika utawala wa Jimbo la Papa na kanisa Katoliki kwa ujumla . Amesema, kwa niaba ya watu wa Italia, na yeye mwenyewwe binafsi , anatoa pongezi za dhati na kumtakia kila la kheri kwa kazi yake mpya.

Na kwamba katika kazi hii nzito aliyokabidhiwa na Baba Mtakatifu Francisko, inaonyesha kutambuliwa kwa kazi zake, katika kulihudumia kanisa. Na katika miaka yake mingi alimo hudumia Sekretarieti ya Nchi, utendaji wake uliweza kumulikia vyema maangalisho na tahadhari za mara kwa mara juu ya mahusiano kati ya serikali ya Italia na Jimbo Takatifu, ahadi zake katika ufanikishaji wa maridhiano na makubaliano ya pamoja kati ya nchi hizi mbili, viliwezesha kujenga mshikamano na usawa, katika uhuru kamili kwa pande hizi mbili.

Rais Napilitano , ameonyesha imani yake kwamba kwa uwepo wake kama katibu wa nchi wa Jimbo la Papa , mahusiano kati ya nchi hizi mbili yataendeela kuchanua katika utajiri na mambo mapya na ushirikiano, na hasa ulinzi wa amani na haki kwenye soko la kimataifa, vitazidi kuimarishwa.
Kwa hisia hizo na kwa matumaini ya kukutana hivi kaaribuni, Rais Napolitano, aliridhia kumtumia pongezi na salaam hizi , na kumtakia maisha bora , mafanikio na ustawi binafsi katika utendaji wa ofisi yake mpya ya ngazi ya juu kabisa.
Roma 31 Augosti 2013.








All the contents on this site are copyrighted ©.