2013-08-29 14:58:20

Papa Francisko afungua Mkutano Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Augustine kwa Ibada ya Misa.


Vuguvugu la upendo, huusukuma moyo kupenda kuhudumia wengine kwanza. Na pia roho ya kutaka kujua zaidi, huongoza kwa Mungu na katika kupenda. Ni ujumbe wa Papa Francisko, katika homilia yake, wakati akiongoza Ibada katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Augostine hapa Roma, kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Augustine.

Ibada hiyo iliyohudhuriwa na wanashirika wa Mtakatifu Augustine kutoka bara tano za Dunia,wakiwa ni watawa na walei walio weka maisha yao wakfu kwa mujibu wa karama za Mtakatifu Augostine, ambao wako hapa Roma kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Augustine, unao fanyika hapa Roma.

Papa kabla ya kuingia katika Kanisa Kuu, alisalimia maelfu ya watu waliokuwa wamesimama mitaani, kumlaki. Na aliwataka wote, kusikiliza hamu za moyo zinazotafuta kumjua Kristu na haja ya kuitikia kwa upendo, uwepo wa mahitaji ya wengine.
Katika homilia yake alihoji ni hali zipi zinazoweza kuwa kigezo muhimu katika kudumisha maisha yetu kwa mujibu wa karama za Mtakakatifu Augustine. Alieleza kuwa, ni roho hiyo ya mahangaika ya Augustine,ambayo hata leo hii inatufundisha maana ya roho hiyo ya wasiwasi na mahangaiko ya kumtafuta Mungu.

Papa Francisko alisisitiza kwa kuyakukumbuka maisha binafsi yenye mhemko wa tafiti aa Mtakatifu Augostine,tunaopata kufahamu kwamba kuna mambo matatu nayo ni harara na Wasiwasi za kiroho , kutafuta kukutana na Mungu na hamu ya kupenda wengine.

Alisema, wale wanaokuwa kinyume na Mungu na imani , wale ambao wako mbali na Mungu au walio telekeza imani, na pia kwetu tunaojiweka mbali na kuwa utoro kwa Mungu , katika maisha ya kila siku, kwa mtazamo wa kina ndani mwetu wenyewe, tunapaswa kujiuliza ni ipi hamu kuu ya moyo , au tuna roho aliyelala tu bila kujali yanayoendelea katika maisha yetu.

Tunapaswa kuwa na moyo wa kutotulia kama wa Mtakatifu Augustine, roho ya wasiwasi iliyo mwongoza hadi kukutana na Kristo. Hamu ya moyo usiotaka kujifungia wenyewe binafsi.

Papa aliendelea kusema, na hata katika gunduzi za kukutana na Mungu , Mtakatifu Augustine, Askofu wa Ipponea, hakusimama hapo, bali aliendelea kutembea katika njia ya kumtafuta Mungu bila kuchoka. Kutotulia katika kuutafuta ukweli. Hivyo kumtafuta Mungu, inakuwa ni utendaji wa kila siku unaotaka kujua mengi zaidi na kutenda kwa ajili ya wengine. Na hiyo ndiyo hamu ya upendo wa kweli kwa wengine.

Alisisitiza Papa Francisko na kusema hamu hiyo, inapaswa kuwa tabia ya kichungaji, kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Augostine ya kumtafuta Mungu daima, kumtangaza Kristu kwa ujasiri na bila woga, na kuivaa sura ya Yesu Mchungaji mwema ambaye huwajua kondoo wake (taz. Yn 10:14) ,

Papa pia aliwatazamisha katika wasiwasi na hofu za Mtakatifu Monica Mama yake Augostine, jinsi alimvyomwaga machozi yake akiomba uongofu wa mwanae ! Na jinsi mama wengi leo , pia wanavyo mwaga machozi yao kwa sababu ya kutaka watoto wao warudi kwa Kristo! Papa alihimiza hili na liwe somo la kutopoteza matumaini katika neema ya Mungu!

Francisko, Papa alihitimisha hotuba yake, kwa kumwomba Bwana, ili pia atujalie sisi roho hiyo ya kutotulia katika kumtafuta Mungu na kuishi nae na pia kwa ajili ya kupata ujasiri wa kutangaza upendo wa Mungu kwa kila mke na mme bila kuchoka.








All the contents on this site are copyrighted ©.