2013-08-29 15:05:41

Papa awaasa vijana kuwa wajenzi wa mazuri, fadhila na ukweli


Papa Jumatano Papa alikutana na kikundi cha vijana wapatao mia tano wa jimbo la Piacenza -Bobbio Italia, wakiongozwa na Askofu Gianni Ambrosio wa jimbo la Piacenza. Vijana walikuwa katika hija ya ya kutembelea kitovu cha kanisa, kama sehemu ya maadhimisho ya mwaka wa Imani .

Katika hotuba yake, Papa aliwaambia vijana kwamba, wana hazina ya matumaini katika mioyo yao. Na ni wawasilishaji wa tumani , kwa kuwa wao ndiyo wanayaishi maisha ya sasa na ni watengenezaji wa hali ya baadaye . Ni watendaji wakuu wa sanaa ya maisha ya baadaye.

Papa alieleza na kutaja shauku za vijana wengi kwamba ni uzuri, wema na ukweli. Na kwamba hamu hizo zimeandikwa ndani ya mioyo yao, na wanapaswa kuzikumbatia wakati wanasonga mbele ya maisha, hasa katika kuyajenga maisha bora ya baadaye.

Ujana ni wakati wa kuyaishi maisha ya sasa na pia ni kwa ajili ya kujenga maisha ya baadaye. Na hivyo inakuwa ni changamoto kwao, lakini kwa ujana una uwezo wa kupambana na kupata ushindi, iwapo hawatazembea na kumwacha mwovu kuvuruga hamu halisi za moyo. Hivyo ni kuwa na ushupavu na kusonga mbele na hamu hiyo ya kuyatengeneza maisha mazuri , fadhila na ukweli.


Na hii inamaanisha ni kupigia kelele dhidi maisha yanayoharibu ustaraabu wa uzuri, fadhila na ukweli. Ni kwenda kinyume na wimbi la hatari la kupenda malimwengu yenye kuangamiza mwili na roho pia. HIvyo Papa alihimiza, vijana wasonge mbele kwa kutamani mazuri, mema na ukweli.

Askofu Gianni Ambrosio wa Jimbo la Piacenza Bobbio, ameonyesha tumaini lake kwamba, vijana kukutana kwao na Papa wameweza kuchota chochote kwa ajili ya maisha yao ya Kikristu. Na hivyo anawatazamia watakuwa ni mwanga na chachu katika kuboresha maisha ya vijana Jimboni Piacenza.


Na aliwaambia vijana kwamba, tukio la kufanya hija katiak madhabahu ya Mtakatifu Petro na kukutana na Papa katika hija hii, muhimu kwanza kabisa,inakuwa nimwanga wa kuwaangazia katika njia yao ya maisha. Ni kupata ufahamu kwamba, maisha yetu humulikiwa na mwanga wa uwepo wa Kristu Mfufuka ambaye daima huandamana na wale wanaompokea katika mioyo yao na kuishi nae. Na kwa namna hiyo Kanisa linaendelea kuwepo na kutimiza utume wake wa kuifikisha habari njema ya upendo wa kuokoa kwa watu wote.

All the contents on this site are copyrighted ©.