Italia haitashiriki kwenye mashambulizi ya kisilaha dhidi ya Syria ikiwa Umoja wa
Mataifa hautahusika kwenye mashambulizi hayo. Haya yamesemwa na Waziri Mkuu wa Italia
Bw. Enrico Letta kwenye mahojiano na Radio Anchiāio yenye kurushia matangazo yake
mjini Roma. Hata hivyo, amesema Waziri Mkuu Letta kwamba nchi yake inalaani vikali
vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na serikali ya rais Bashar Assad wa Syria dhidi
ya wananchi wa Syria.
Hapo awali rais Barrack Obama wa Marekani alinukuliwa
na Shirika la Habari la AP akisema kwamba nchi yake imethibitisha kwamba serikali
ya Assad ndiyo iliyohusika na mashambulizi ya kikemikali ya hivi karibuni yaliyosababisha
vifo vya watu karibiya 100 nchini Syria. Marekani inasema kuna haja ya jumuiya ya
kimataifa kuingilia kati ili kuithibiti serikali ya Bashar Assad dhidi ya kutumia
silaha za kemikali kwani shambulizi la aina hii lina athari ya kimataifa.
Waziri
mkuu wa Italia Bw. Enrico Letta hata hivyo ameiomba jumuiya ya kimataifa kuchukua
tahadhari kubwa katika kuingilia kati mzozo wa Syria. Italia na mataifa mengine ya
Ulaya yanachukua tahadhari hiyo kwani bado kuna utata juu ya nani hasa kaagiza utumiaji
wa mashambulizi kwa kutumia silaha za kikemikali nchini Syria.
Baba Mtakatifu
Francisko kwenye ujumbe wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter siku ya Alhamisi
anasema kwamba Upendo wa Mungu sio kitu cha hewani, ila ni kitu chenye jina na sura:
Yesu Kristo. Hivyo ni mwaliko kwa jumuiya ya kimataifa kuona sura na jina la Yesu
Kristo ndani ya watu wote wanaoteseka na kuchukua hatua ambazo zitaisadia nchi ya
Misri kumaliza vurugu na kinzani za kivita zinazoendelea nchini humo,
Jumuiya
ya kimataifa inapoamua kuingilia kati mgogoro wa Syria, inapaswa kuchukua tahadhari
kubwa na kuonyesha upendo mkuu kwa wananchi wa Syria wasio na hatia na wanaoendelea
kuteseka kwani wanajikuta katikati ya vita na kinzani wasichokielewa.