2013-08-28 11:26:25

Mfalme wa Jordan kumtembelea Papa -Vatican


Alhamis August 29, Mfalme Abdullah II Ibn Hussein wa Himaya ya Ufalme wa Jordan, atamtembelea Papa Francisco katika makazi yake ya Vatican. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hao mashuhuri kukutana. Mfalme Abdullah 11, aliwahi kukutana na Papa Benedict XVI mnamo May 2009 mjini Amman, wakati Papa alipofanya ziara yake ya kitume katika nchi Takatifu,na alifika mto Jordan.

Nchi ya Jordan alikobatizwa Yesu, ni nchi dogo katika eneo la Mashariki ya Kati , nchi ya Kiarabu ambako kuna kingo za mto Jordan na nchi yenye kuwa na historia za kale katika mkoa wa Palestina. Na hupakana na Kusini na Mashariki na, Upande wa KaskanzIni Mashariki, Kaskazini na upande wa Magharibi , ambako hushirikishana udhibiti wa Bahari ya Shamu .

Jordan ina idadi ya watu million 6, 249, 000, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011.
Ufalme huu katika eneo la jangwa uliibuka baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia, iliyotenganisha eneo la Asia Magharibi kwa juhudi za Uingereza na Ufaransa. Na mwaka 1946, Jordan ikiwa taifa huru la kujitegemea na kujulikana kama Ufalme wa Hashemite wa Jordan. Na baada ya vita vya mwaka ,Mfalme wa Abdullah I, alilitwaa tena eneo hilo na kujulikana kama Ufalme wa Jordan kunako 1949.

Jordan hutetea uhuru wa kidini, ingawa Uislamu ni dini inayojulikana kuwa rasmi kiserikali na asilimia 92% ya Waislamu ni wa dhehebu la Sunni. Na kuna udhaifu katika utendaji wa kuhakikisha uhuru wa kidini kwa watu, Muislamu anayeamua kuongokea dini nyingine hupambana na sheria kali za kijamii na hubaguliwa kisheria.








All the contents on this site are copyrighted ©.