2013-08-27 15:26:15

Ujumbe wa Papa katika Sura ya Nne ya mwanga wa Imani


Monsinyori John Kennedy, Afisa katika Shirika la Kipapa kwa ajili ya Mafundisho Sadikifu ya Kanisa, akiitafakari sura ya mwisho ya waraka wa Mwanga wa Imani , uliotolewa na Papa Francisko, amesema sura hii imejikita zaidi katika Barua kwa Waebrania, ambamo mnaelezwa jinsi Mungu, alivyowaandalia wana wa Isreal, mji kwa ajili yao. Na hivyo ni habari njema kwa watu wote.
Mons. Kennedy anasema, Papa Francisko akiwarejea Wakuu wa Makanisa na haki za wake kwa waume wa wakati wa Agano la Kale, anaitaja barua kwa Waebrania, kwamba, ina vigezo maalum katika imani, kwamba, imani si tu huwasilishwa kama njia, lakini pia kama utaratibu wa kujenga, ambao daima huanza na maandalizi ya mahali ambamo binadamu anaweza kuishi kwa ushirikiano na wengine.
Na mfano umetolewa kama Noah alivyoandaa safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Na Abraham alivyoandaa kuishi katika mahema, wakati akisubiri kwenda katika nchi ya ahadi kwa matumaini makubwa.
Kwa muono huo, Monsinyori Kennedy anaendelea kusema, Papa Francisko katika sura hii, pia anaonyesha kwamba, uthabiti katika imani, huweka alama za maandalizi ya kuelekea katika mji wa ahadi unaoandaliwa na Mungu kwa binadamu. Na kwa kutambua hili, tunaweza kuona kwamba, kwa kila binadamu , imani humwangazia binadamu juu ya mahusiano yake na Mungu. Na ndani mwake huzaliwa upendo na tafakari zaidi za kuuona upendo huo wa Mungu mwenyewe. Mungu mwenyewe amini, anaye wapatia waamini wake mji, mji wa matumaini, usiokuwa na miisho.

Mons Kennedy, anaendelea kuangalisha katika maisha ya kila siku na matokeo yake anasema, hili ni dhahiri, kama alivyosema Papa Francisko kwamba, mwanga wa imani , unadai kuwekwa katika huduma ya sheria ya haki, na amani, mwanga huo unakuwa ni uwezo unaoongeza nguvu katika mahusiano ya binadamu, na katika kuboresha maisha ya pamoja na mshikamano wa kijamii.

Imani inafanya sisi kufahamu usanifu wa mahusiano kati ya binadamu kwa sababu imani huzingatia msingi ya adilifu katika muono wa sheria za Mungu. Na hivyo imani inakuwa huduma kwa manufaa ya wote.

Papa Francis kisha anasema, imani si tu huangazia a mambo ya ndani ya Kanisa, au kutumika tu katika kujenga mji wa milele, lakini pia husaidia kujenga jamii yetu katika njia ya uhakika kwa jamii, kutembea vyema kuelekea mustakabali wa maisha yenye matumaini.

Anaendelea kuangalisha katika manufaa ya familia na jamii , kwamba, kuirejesha imani katika familia, inakuwa ni uwasilishaji wa uwezo wa mwanga, wenye kumulikia mahusiano katika jamii nzima. Ni kuiwezesha familia na jamii kufanya majiundo adilifu na manufaa ya wote. Huanzia katika jamii kutembea katika njia ya udugu, kwenye muono kwamba, sisi sote ni wana wa Baba Mmoja wa mbinguni.







All the contents on this site are copyrighted ©.