Ni vigumu kunyamalia kilio cha watoto wahanga Syria Mons. Zenari
Akihojiwa na Redio Vatican juu ya vitendo vya kutisha vinavyoendelea Syria, Mjumbe
wa Papa wa Damscus, Askofu Mkuu Mario Zenari, anasema, katika siku za hivi karibuni
, ambako kumekuwa na utendaji wa kinyama kwa watoto wasiokuwa na hatia, ni vigumu
kunyamalia kilio cha watoto hao, kinachoililia mbingu na jumuiya ya kimataifa, kuona
mateso na mahangaiko yao. Ameserma ni wazi, katika siku hizi, wanainua zaidi sauti
katika sala kuomba jumuiya ya kimataifa iwajibike zaidi,na kutumia busara zaidi, ili
kupata jawabu linalo faa kusitisha kipeo hiki cha syria. Jumuiya ya Kimataifa inapaswa
kutoa jibu haraka lakini makini, ili uharifu na unyama huu kamwe usipate kujirudia
Syria, Na akijibu swali juu ya utumiaji wa silaha za kemikali, amesema, jumuiya
ya kimataifa inapaswa kuthibitsha ukweli wa taarifa zinazotolewa kwamba, silaha za
kemikali zimetumika na pia kuingilia kati kuhakikisha utawala mahalia, unatoa ushirikiano
wa kutosha kwa hoja hii, pia kwa pande zote zinazo husika katika mzozo huo.
Askofu
Zenawi, ameitaka jumuiya ya Kimataifa itende kwa haraka, kufanikisha maridhiano ya
kitaifa kwa ajili ya kukomesha machafuko hayo.