2013-08-24 11:41:12

Jitokezeni kwa wingi ili kuombea amani duniani hapo tarehe 21 Septemba 2013


Baraza la Makanisa Ulimwengu linawaalika Makanisa wanachama kuhakikisha kwamba, yanashiriki kikamilifu katika Siku ya Kuombea Amani Kimataifa, itakayoadhimishwa hapo tarehe 21 Septemba 2013. Kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho haya ni "Mungu wa uhai, tuongoze katika haki na amani".

Baraza la Makanisa Ulimwengu litafanya kumbu kumbu hii kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa. Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwepo na matukio sehemu mbali mbali za dunia yanayoonesha uvunjifu wa misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano kati ya watu; mambo ambayo yanaendelea kusababisha mateso na mahangaiko makubwa kwa watu.

Sala ni silaha madhubuti katika kupambana na malimwengu. Siku ya kuombea amani kimataifa ilianzishwa kunako mwaka 2004 baada ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kukubaliana na kimsingi na ombi lililotolewa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni.All the contents on this site are copyrighted ©.