Viongozi mbali mbali wa Kanisa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mwishoni mwa Juma
walilazimika kuzikimbia Parokia na Nyumba zao za Kitawa kwa kuhofia usalama wa maisha
yao baada ya Jeshi la Seleka kuanzisha mashambulizi katika maeneo kadhaa nchini humo.
Hivi karibuni kiongozi wa kikundi cha Waasi cha Seleka aliapishwa kuwa ni
Rais wa Jamhuri ya watu wa Afrika ya Kati.