2013-08-23 08:13:25

Zimbabwe na awamu nyingine tena ya uongozi!


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Alhamisi amekula kiapo cha kuwaongoza wananchi wa Zimbabwe kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Sherehe hii imeongozwa na Bwana Godfrey Chidyausiku, Jaji mkuu wa Zimbabwe na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi wa Zimbabwe.

Rais Mugabe aliwaongoza wananchi wa Zimbabwe kujipatia uhuru wao kunako mwaka 1980, akaapa kutetea masilahi na haki za wananchi wanyonge nchini Zimbabwe.

Katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mugabe, Chama Kikuu cha Upinzani, hakikuhudhuria kwa madai kwamba, uchaguzi hakuwa huru wala wa haki na kwamba, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni za uchaguzi, tuhuma ambazo zimetupiliwa mbali na Mahakama kuu ya Zimbabwe na hivyo kuhalalisha ushindi wa Rais Mugabe katika uchaguzi mkuu uliofanyika hapo tarehe 31 Julai 2013.

Sherehe hizi zimehudhuriwa na viongozi kadhaa kutoka katika nchi za SADCAll the contents on this site are copyrighted ©.