2013-08-20 11:57:52

Vikwazo vya kiuchumi bado vina athari kubwa nchini Zimbabwe


Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC inazitaka nchi za Magharibi zilizokuwa zimeiwekea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi kuangalia tena msimamo wao baada ya Zimbabwe kufanikisha uchaguzi ambao umekuwa "huru na wa amani". Wananchi wa Zimbabwe wameteseka kwa muda mrefu kutokana na vikwazo vya kiuchumi baada ya kuibuka kwa machafuko ya kisiasa nchini humo yaliyopelekea kuundwa kwa Serika ya Umoja wa Kitaifa.

Changamoto hii imetolewa hivi karibuni na Rais Joyce Banda wa Malawi ambaye kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa SADC. Nchi nyingi za Ulaya bado zinasema kwamba, ni mapema mno kuiondolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi kutokana na ukiukwaji wa haki msingi za binadamu ambao umefanyika nchini humo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

SADC inawataka wadau mbali mbali nchini Zimbabwe kujenga mshikamano wa kitaifa kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi wa Zimbabwe na Afrika katika ujumla wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.