2013-08-20 09:55:53

Mtakatifu Stefano wa Hungaria ni rasilimali maadili katika ujenzi wa amani mshikamano na udugu!


Wananchi wa Hungaria tarehe 20 Agosti kila mwaka wanaadhimisha Siku kuu ya Mtakatifu Stefano wa Hungaria, aliyetangazwa kuwa Mtakatifu na Papa Gregori wa VII kunako Mwaka 1083.

Mtakatifu Stefano ni Baba na Muasisi wa taifa la Hungaria, baada ya kumwongokea Mwenyezi Mungu, ujumbe wa Habari Njema ya Wokovu ukaweza kupenya katika mioyo ya wananchi wa Hungaria. Siku hii inaadhimishwa kwa maandamano makubwa huku wakibeba masalia ya Mtakatifu Stefano.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa Rais Jànos Ader wa Hungaria anawatakia kheri na baraka katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Mtakatifu Stefano wa Hungaria amana ya maisha ya kiroho na kiutu; rasilimali maadili katika ujenzi wa Jamii inayosimikwa katika amani, mshikamano na udugu.All the contents on this site are copyrighted ©.