2013-08-20 10:50:00

Misri inapambana dhidi ya vitendo vya kigaidi!


Baraza la Maaskofu Katoliki Misri linasema kwamba, kuna Makanisa 58 na Majengo kadhaa ya Taasisi za Makanisa yamechomwa moto na kuharibiwa vibaya. Kati ya Makanisa 58, yaliyochomwa moto, kuna Makanisa 14 ya Kanisa Katoliki. Makanisa haya yamechomwa moto katika maeneo: Al Minya na Assiut yanayokaliwa na Waislam wenye imani kali.

Baraza la Maaskofu Katoliki Misri linasema kwamba, hii si vita kati ya Waislam na Wakristo, kwani kuna raia wema wa dini zote walioshiriki kusaidia kuzima moto kwa Makanisa yaliyokuwa yanateketea. Kanisa linasema hii si vita ya wenyewe kwa wenyewe bali ni vita dhidi ya vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wa Misri na waamini wenye misimamo mikali ya kiimani.All the contents on this site are copyrighted ©.