Benedikto XVI atembelea Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo
Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita, Jumapili mchana alitembelea kwa
muda mfupi Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo. Akiwa mahali hapo, aliweza kusali Rozari
pamoja na kusikiliza tamasha la muziki lililokua limeandaliwa kwa heshima yake.
Baadaye
jioni, Baba Mtakatifu mstaafu alirejea tena mjini Vatican kuendelea na maisha yake
ya sala na tafakari kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa la Kristo.