2013-08-17 11:25:32

Onesheni mshikamano wa upendo kwa watoto wanokufa kwa njaa!


Baba Mtakatifu Francisko katika mafundisho yake anaendelea kuwahimiza waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuondokana na utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya jirani na badala yake kuanza mchakato wa mshikamano wa upendo na udugu, kwani wote ni watoto wa Mungu, licha ya tofauti zao mbali mbali.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii al maarufu kama twitter anasema, haiwezekani kupata usingizi mnono wakati ambapo kuna maelfu ya watoto wanaofariki dunia kutokana na baa la njaa na utapiamlo wala wazee ambao hawana huduma za afya.

Wachunguzi wa masuala ya mawasiliano ya kijamii wanasema kwamba, Baba Mtakatifu Francsiko kwa sasa anawafuasi wapatao millioni 8 ambao wamejisajili kwenye akaunti yake ya twitter.All the contents on this site are copyrighted ©.