2013-08-13 11:18:45

MDC yafungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu Zimbabwe


Chama cha Upinzani cha MDC kinachoongozwa na Bwana Morgan Tsvangirai, mwishoni mwa juma, kimefungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu kwenye Mahakama kuu nchini Zimbabwe.

MDC kimeamua kufungua kesi Mahakama Kuu baada ya Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe kushindwa kutoa majibu muafaka ya mashaka yaliyooneshwa na Chama hiki pamoja na baadhi ya waangalizi wa kimataifa kusema kwamba, kulikuwa na kasoro katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe, hapo tarehe 31 Julai 2013 na Rais Robert Mugabe kuibuka kidedea.







All the contents on this site are copyrighted ©.