2013-08-12 08:55:12

Waislam na Wakristo wanachangamotishwa kujenga utamaduni wa kuheshimiana kwa njia ya elimu


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili iliyopita, aliwakumbusha waamini na mahujaji waliokuwa wamemiminika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwamba, Alhamisi, tarehe 15 Agosti, 2013, Mama Kanisa ataadhimisha Siku kuu ya Bikira Maria kupalizwa mbinguni: mwili na roho.

Kwa namna ya pekee, Baba Mtakatifu Francisko amewakumbuka waamini wa dini ya Kiislam kutoka sehemu mbali mbali za dunia walioadhimisha Siku kuu ya Id El Fitri hivi karibuni. Anasema, Mfungo mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilikuwa ni fursa makini kwa waamini wa dini ya Kiislam kuweza: kusali, kufunga na kutoa sadaka kwa maskini.

Baba Mtakatifu anawaalika waamini wa dini ya Kiislam na Kikristo kujibidisha zaidi katika kuendeleza mchakato unaopania kujenga utamaduni wa kuheshimiana kwa njia ya elimu hasa kwa vijana wa kizazi kipya, kama alivyofafanua kwa kina katika ujumbe wake kwa waamini wa dini ya Kiislam wakati wa Siku kuu ya Id El Fitri.







All the contents on this site are copyrighted ©.