2013-08-12 12:56:45

Mzee Madiba!


Serikali ya Afrika ya Kusini, Jumapili iliyopita katika taarifa yake kwa vyombo vya habari inasema kwamba, hali ya afya ya Mzee Nelson Mandela, aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini inaendelea kuboreka kwa kiwango kidogo sana.

Mzee Madiba mwenye umri wa miaka 95 anaendelea kupata matibabu mjini Pretoria kwa muda wa miezi miwili kwa sasa. Watu wengi bado wanaendelea kumkumbuka na kumwombea katika sala na dua zao.







All the contents on this site are copyrighted ©.