Mfuko wa Uwezo Kenya, unapania kutoa fursa za ajira kwa vijana
Serikali ya Kenya imeamua kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa wajasiriamali vijana
na wasichana kama sehemu ya mchakato wa kupambana na ukosefu wa ajira pamoja na umaskini
miongoni mwa vijana. Serikali imetenga kiasi cha shilingi za Kenya billioni sita zitakazotolewa
kwenye Mfuko wa Uwezo.
Lengo hili limetangazwa hivi karibuni na Makamu wa
Rais wa Kenya Bwana William Ruto anayekazia kwamba, mfuko wa uwezo utaanza kutoa mikopo
isiyokuwa na riba kuanzia mwezi Septemba baada ya kupokea na kupitisha maombi ya vijana
kutoka sehemu mbali mbali nchini Kenya.
Vijana watapaswa kuitumia fedha hii
kwani watalazimika kuiridisha kadiri ya mkataba. Wale watakaofanikiwa watakuwa na
nafasi nzuri ya kupewa tena mkopo huo.