Serikali ya Namibia inasema kwamba, wananchi wake zaidi ya laki nne wanakabiliana
na baa la njaa kutokana na ukame wa muda mrefu. Namibia inakadiriwa kuwa na watu zaidi
ya millioni mbili. Hali ya sasa ni kama ile iliyojitokeza kunako mwaka 1980, wananchi
wengi wa Namibia walipoteseka kwa baa la njaa.
Serikali ya Namibia inaiomba
Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kuokoa maisha ya wananchi wake wanaokabiliwa na ukosefu
wa chakula kwa sasa. Ukame wa muda mrefu una madhara makubwa kwa maisha na maendeleo
ya wananchi wa Namibia, lakini waathirika wakubwa ni wale wanaoishi vijijini. Ukame
unatishia pia sekta ya utalii ambayo ni chanzo kikuu cha pato la taifa nchini humo.
Ukame unaendelea pia kutishia maisha ya wananchi wa Angola.