Raia wawili wa Uingereza wamwigiwa tindikali Zanzibar
Serikali ya Uingereza imeonesha hali ya wasi wasi baada ya raia wake wawili waliokuwa
wanafanya kazi ya kujitolea Kisiwani Zanzibar kumwagiwa tindikali na hivyo kuwasababishia
majeraha makubwa siku ya Alhamisi, tarehe 8 Agosti 2013.
Hili ni tukio la pili
katika kipindi cha hivi karibuni, kwani Shekhe Fadhili Suleiman, Mwezi Novemba 2012
alishambuliwa na watu wasiojulikana hadi leo hii kwa kumwagiwa tindikali.