2013-08-07 09:36:09

Vita baridi bado inatishia amani ya Jumuiya ya Kimataifa!


Wananchi wa Japan, tarehe 6 Agosti 2013 wamefanya kumbu kumbu ya miaka 68 tangu mji wa Hiroshima uliopolipuliwa kwa bomu la atomic na kusababisha vifo vya watu 70, 000 kwa mkupuo na wengine wengi kuendelea kufariki dunia baadaye. Wawakilishi kutoka katika nchi 74 wamehudhuria tukio hili, changamoto kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha kwamba, inakuwa huru dhidi ya vitisho vya umilikaji na matumizi ya silaha za kinyuklia.

Hii ni changamoto ambayo imetolewa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki-Moon wakati wa kumbu kumbu ya miaka 68 ya shambulizi la atomic kwenye mji wa Hiroshima. Jamii ya kimataifa bado imekumbwa na hofu ya vita, dalili kwamba, hata leo hii bado kuna vita baridi inayoendelea chini kwa chini.







All the contents on this site are copyrighted ©.