2013-08-07 12:12:43

Uwanja wa Jomo Kenyatta Kenya wafungwa kutokana na ajali ya moto!


Serikali ya Kenya siku ya Jumatano imelazimika kuufunga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta baada ya moto kutokea kwenye uwanja huo mapema Jumatano asubuhi na hivyo kusababisha hasara kubwa. Hakuna mtu aliyejeruhiwa kutokana na kuzuka kwa moto huo ingawa umesababisha usumbufu na hasara kubwa kwa wasafiri na wafanyabiashara ndani na nje ya Kenya.

Uchunguzi wa awali unaonesha kwamba, moto huo umesababishwa na milipuko miwili, kadiri ya taarifa iliyotolewa na Reuters. Serikali ya Kenya inaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha moto huo ambao umesababisha usumbufu kwa wasafiri na watalii wengi wakati huu wa msimu wa utalii kwa nchi za Afrika ya Mashariki. Kutokana na moto huo mashirika kadhaa ya Ndege yamefuta safari zake kwenda Kenya.







All the contents on this site are copyrighted ©.