2013-08-07 11:05:57

Rais Mugabe aibuka kidedea, Tsvangirai asusia matokeo!


Tume ya Uchaguzi Zimbabwe imemtangaza Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika kunako tarehe 31 Julai 2013. Rais Mugabe ameibuka na ushindi kwa asilimia 61% ya kura zote halali zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake Waziri mkuu wa zamani Morgan Tsvangirai aliyepata asilimia 34% ya kura zote halali zilizopigwa.

Rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF wamepata viti 160 vya wabunge na Chama cha Tsvangirai, MDC kimejipatia viti 49. Bwana Tsvangirai anapinga matokeo ya uchaguzi mkuu kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza katika mchakato mzima na kwamba, kuanzia sasa wataanza kwenda mitaani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu. Viongozi kadhaa kutoka Afrika wamemtumia Rais Mugabe salam za pongezi kwa kuibuka kidedea katika uchaguzi huu ambao sasa unaonekana kuwa na utata!







All the contents on this site are copyrighted ©.