2013-08-07 12:00:19

Jitihada za kujenga na kudumisha amani kwa njia ya majadiliano Nigeria bado zinakumbana na vikwazo kibao!


Nchi ya Nigeria bado haijapata suluhu ya kuleta amani kwenye maeneo yake yaliyokumbwa na vita kinzani na vurugu za kidini zinazosababishwa na kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram.

Kuibuka kwa migogoro kwenye majimbo mbalimbali kaskazini mwa Nigeria kwenye miezi ya hivi karibuni hakuonyeshi jitihada ya Serikali inayopania kudhibiti vitendo vya kigaidi Kaskazini mwa Nigeria pamoja na kuendeleza mchakato wa majadiliano ya kidini, kijamii na kitamaduni nchini humo.

Watu wengi bado wana chuki, uhasama na hali ya kutaka kulipizana kisasi, jambo ambalo ni hatari kwa maisha, ustawi na maendeleo ya wananchi wa Nigeria. Mwishoni mwa juma, watu 35 wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na Kikundi cha Boko Haram. Wananchi na watu wote wenye mapenzi mema bado wanaendelea kuhimizwa kusimama kidete kulinda na kutetea uhai ambayo ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Bara la Afrika halina budi kuachana na sera za chuki na misimamo mikali ya kiimani kwani mambo haya ni vikwazo vikubwa vya maendeleo na ustawi wa taifa lolote lile! Ikumbukwe kwamba, amani ni jina jipya la maendeleo.









All the contents on this site are copyrighted ©.