2013-08-06 10:55:15

Mwanga wa imani unaangazia mahusiano ya upendo ili kuishi na kupenda kama Kristo mwenyewe!


Mwanga wa Imani ni Waraka wa kwanza kutolewa na Baba Mtakatifu Francisko, katika mwendelezo wa Maadhimisho ya Mwaka wa Imani. Waamini wameaminishwa katika upendo wa Mungu, kwani bila imani hawawezi kufanikiwa kuyaelewa Mafumbo na Kweli za Kiinjili.

Mama Kanisa anarithisha kwa watoto wake imani ambayo amepokea kutoka kwa Kristo mwenyewe katika Sakramenti, Sala na Amri za Mungu. Waamini wanakumbushwa kwamba, imani ni mafao ya wengi na Bikira Maria ni mfano na kielelezo cha mwamini wa kweli.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, mwanga wa imani unaangazia mahusianno ya watu na kuwasaidia waamini kuishi katika umoja na mapendo kwa Kristo kama Kristo mwenyewe alivyoishi.







All the contents on this site are copyrighted ©.