2013-08-05 10:47:01

Miaka 35 tangu alipofariki Mtumishi wa Mungu Paulo VI


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili iliyopita alikumbusha kwamba, tarehe 6 Agosti 2013, Kanisa litafanya kumbu kumbu ya miaka 35 tangu Mtumishi wa Mungu Papa Paulo wa VI alipofariki dunia, akiwa kwenye Ikulu Ndogo ya Castel Gandolfo, nje kidogo ya mji wa Vatican.

Askofu Francesco Beschi wa Jimbo Katoliki Bergamo, Italia anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican majira ya jioni. Sr. Gisela Upendo Msuya anatujuza kwa ufupi historia na mchango wa Mtumishi wa Mungu Papa Paulo wa VI. RealAudioMP3All the contents on this site are copyrighted ©.