2013-08-05 14:15:40

Jaji Francis S. K. Mutungi ateuliwa kuwa ni Msajili mpya wa Vyama vya Siasa Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
All the contents on this site are copyrighted ©.