2013-08-03 15:08:07

Hali ya wasi wasi inazidi kuongezeka huko Syria!


Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki anaungana na viongozi wa Mashirika ya Makanisa ya Mashariki kuonesha moyo wake wa mshikamano na Wayesuit wote kutokana na wasi wasi wa kupotea katika mazingira tata Padre Paolo Dall'Oglio.

Baraza la Kipapa bado linaendelea kusali na kuwambuka pia Maaskofu wawili na Mapadre wawili kutoka Mashariki waliotekwa nyara hadi sasa hawajulikani mahali walipo. Kardinali Sandri anasema, anawakumbuka hata wananchi wengine wote wa Syria na wageni ambao wanaendelea kupotea katika mazingira tata. Kardinali Sandri anaendelea kusali ili amani iweze kurejea tena huko Syria na Mashariki ya Kati.All the contents on this site are copyrighted ©.