2013-08-02 15:23:51

Fuateni sheria, kanuni na miongozo ya Liturujia ya Kanisa


Baba Mtakatifu Francisko anatarajia hivi karibuni kuchagua kiongozi wa kitume atakayefuatilia masuala ya: maisha, uongozi, utume na liturujia inayoadhimishwa na Shirika la Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili.

Ufafanuzi huu umetolewa na Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican na kukazia kwamba, Baba Mtakatifu anawataka Watawa hawa kuadhimisha Mafumbo ya Kanisa kadiri ya sheria na kanuni za Kanisa kama zilivofafanuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita. Hakuna sababu ya kuwa na mkanganyo katika Maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu wala kuwa na kinzani katika masuala haya. Sheria, kanuni na taratibu zinapaswa kufuatwa kikamilifu.All the contents on this site are copyrighted ©.