Baba Mtakatifu Francisko anawaambia vijana mara baada ya Maadhimisho ya Siku ya 28
ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 iliyosheheni utajiri mkubwa wa maisha ya kiroho,
kiutu na kitamaduni, sasa kuanza kumwilisha yote waliyoungama wakati wakiwa Rio de
Janeiro.