2013-07-29 08:52:16

Pokeeni zawadi ya maisha kwa moyo wa shukrani na mapendo!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi mara baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu kwa Makleri na Watawa, wakati akitoka Kanisani alikutana na Familia moja iliyokuwa imebeba mtoto ambaye alizaliwa bila ubongo, watoto ambao mara nyingi hufariki dunia maramoja! Wazazi hawa kwa utashi wao wenyewe wameamua kuipokea zawadi ya maisha, kuitunza na kuiendeleza hadi pale Mwenyezi Mungu atakavyo amua mwenyewe.

Padre Federico Lombardi anasema, tukio hili limemgusa kwa namna ya pekee Baba Mtakatifu Francisko kiasi kwamba, wazazi na mtoto wao wamealikwa kushiriki katika matoleo na Baba Mtakatifu mwenyewe amempokea mtoto huyu mikononi mwake wakati wa matoleo, changamoto kwa waamini na watu wenye mapenzi mema kupokea na kuitunza zawadi ya maisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.







All the contents on this site are copyrighted ©.