2013-07-29 10:22:32

Kardinali Tonini, mtu wa watu afariki dunia akiwa na umri wa miaka 99


Kardinali Ersilio Tonini, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Ravenna-Cervia amefariki dunia hivi karibuni akiwa na umri wa miaka 99. Ni kiongozi aliyefahamika sana kwa msimamo wake wa kutetea wanyonge ndani ya Jamii, mtu mwenye imani thabiti katika hija ya maisha yake ya kiroho. Alibahatika kujaliwa hekima na ujasiri, uliomwezesha kukutana na kuzungumza na watu wengi.

Kardinali Tonini alizaliwa kunako tarehe 20 Julai 1914 alipadrishwa kunako mwaka 1937. Mtumishi wa Mungu Papa Paulo wa sita kunako mwaka 1969 akamteuwa na kumweka wakfu kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Macerata na Tolentino na miaka sita baadaye, akateuliwa kuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Ravenna na Cervia. Kunako mwaka 1990 akang'atuka kutoka katika shughuli za uongozi. Kunako tarehe 26 Novemba 1994, Mwenyeheri Yohane Paulo wa Pili akamteuwa kuwa Kardinali.







All the contents on this site are copyrighted ©.