2013-07-25 09:28:46

Rio de Janeiro, kumekucha!


Ijumaa, tarehe 26 Julai 2013, Baba Mtakatifu ataianza siku hii kwa Ibada ya Misa Takatifu na baadaye atashiriki katika kuwaungamisha baadhi ya vijana watakaoshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani. Tukio hili linafanyika kwenye Uwanja wa Quinta da Boa. RealAudioMP3

Atasalimiana na baadhi ya vijana wanaotumikia adhabu yao gerezani na mchana atasali na vijana Sala ya Malaika wa Bwana. Mchana atapata fursa ya kukutana na kuzungumza na Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Vijana na Wafadhili. Siku hii itapambwa kwa vijana kupata chakula cha mchana na Baba Mtakatifu Francisko. Jioni vijana watashiriki pamoja na Baba Mtakatifu kuadhimisha Njia ya Msalaba kwenye ufuko wa Copacabana.








All the contents on this site are copyrighted ©.