2013-07-24 08:21:06

Yanayoendelea kujiri huko Rio de Janeiro


Alhamisi, tarehe 25 Julai 2013, Baba Mtakatifu ataanza siku kwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye makazi yake ya muda hapo Sumarè mjini Rio de Janeiro. Asubuhi atakaribishwa na kupewa ufunguo wa mji wa Rio de Janeiro pamoja na kubariki bendera za Olympic. RealAudioMP3

Atatembelea Jumuiya ya Varginha na baadaye jioni, hapo shughuli ya kuwakaribisha vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia, itaanza kucharuka, kiashilio cha Ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013. Shughuli hii itafanyika kwenye ufukwe maarufu wa Copacabana ulioko mjini Rio de Janeiro.








All the contents on this site are copyrighted ©.